Navigation

Chuo cha Ufundi Mlandizi ni chuo kinacholenga kuwapa walemavu wa akili misingi ya kupata ajira au ya kujitegemea na hivyo kuchangia katika maendeleo ya taifa. Chuo bado kipo kwenye ngazi ya ujenzi.

Ni mradi unaoendeleza kazi ya Kituo cha Diakonia cha Mtoni penye shule ya watoto wenye ulemavu wa akili. Baada ya kumaliza shule mara nyingi walikosa njia za kuendeleza maisha yao wenyewe. Chuo cha Ufundi Mlandizi ni taasisi ya kwanza Tanzania inayoandaa watu wenye  ulemavu wa akili kwa maisha ya kujitegemea katika mazingira ya kisasa.

Anuani

S.L.P: 837 Dar es Salaam
Eneo: Mlandizi, Kibaha
-6.753972, 38.746917