Navigation

WAJIBU NA MAJUKUMU YA KITENGO CHA THEOLOJIA:
* Kuratibu utafiti wa masomo ya Mungu na imani ya kikistro,
* Kutoa msaada katika kuelewa vitabu vitakatifu na Maandiko,
* Kutoa msaada wa kitaalamu kwa viongozi wa dini katika kuendeleza ufahamu mpana zaidi wa majukumu yao na kazi
* Kuratibu kuajiriwa kwa Wachungaji,
* Kuratibu maandalizi ya kalenda za matukio ya kikistro.
WAJIBU NA MAJUKUMU YA KITENGO CHA IMANI YA KIKRISTO:
* Kuratibu maendeleo ya mitaala na kosi zilizopo kwa ajili ya mafundisho ya elimu ya kikistro, kozi na semina.
* Kuratibu Mipando na utekelezaji wa programu kwa ajili ya mafundisho ya dini katika shule na vyuo kwa madhumuni ya kukuza ustawi wa kiroho.
* Kuratibu uendelezaji wa madarasa ya kujifunza Biblia katika Sharika na Mitaa.
* Kuratibu mafundisho ya dini katika Shule za jumapili zilizopo kwenye Sharika na Mitaa, pamoja na Shule za Msingi na Sekondari na katika Taasisi za elimu ya juu.
* Kutoa msaada katika kukuza programu maalumu ya Vijana, kwa lengo la kuwaandaa vijana katika kutokomeza umaskini, kwa mfano shughuli za uzalishaji mali.
* Kuandaa na kusimamia Mipango yenye lengo la kuwaandaa Vijana kuwa raia wema na raia wajibikaji wa kikisto.
WAJIBU NA MAJUKUMU YA KITENGO CHA MISIONI NA UINJILISTI:
* Kukuza na kuwezesha kueneza Injili,
* Kuimarisha Waumini kwa lengo la kukuza ukuaji wa kiroho,
* Kukuza ubora katika huduma ya Uchungaji,
* Kuratibu ufunguzi wa maeneo mapya kwa ajili ya kazi ya Utume.
* Kuratibu mahusiano na ushirikiano wa Dayosisi
Anuani
- Simu: Telephone +255 222 113 246
- Simu: Telefax +255 22 2125505
Osifi Yetu
Jina | Cheo | Barua pepe | Simu |
---|---|---|---|
Mch. Boniface Adam Kombo | Naibu Katibu Mkuu Theolojia, Misioni na Uinjilisti | dgsmissions@elctecd.org | +255 222 113 246 |
Mch. Joseph Anael Mlaki | Mratibu wa Elimu ya Kikristo | jmlaki75@gmail.com | +255 784 708 160 |