Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (DKMS), Dkt. Msafiri Mbilu leo Disemba 15, 2020 ametembelea ofisi za Upendo Media zilizopo Posta jijini Dar Es Salama.

Dkt. Mbilu ambaye aliambatana na familia yake, amewatakia Wakristo na Watanzania wote baraka za Mungu katika Christmas pamoja na mwaka mpya 2021.

Dkt. Mbilu amechaguliwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni huko Lushoto Tanga.